MARAFIKI NI WABAYA SANA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

HII MADA NIMEIPATA KWA RAFIKI YANGU MMOJA KULE JF NA NIMEONA NI BORA NIKAISHARE HAPA ILI KUTOA SOMO KWA WAPENZI WENGI AMBAO WALIKUWA HAWANA ELIMU YA NAMNA HII
Katika mahusiano ya mapenzi yoyote kuna watu wanaitwa MARAFIKI. Kabla sijaendelea sana ni vizuri kujiuliza kuna umuhimu gani wa kuwashirikisha marafiki katika mahusiano yako? Mahusiano mangapi yamevunjika kwa sababu ya marafiki ingawa kuna mahusiano yaliyojengwa na marafiki japokuwa ni machache kuliko yale yanayovunjika.

Kuna baadhi ya watu hawawezi kufanya kitu chochote na mpenzi wake bila kumshirikisha rafiki lakini swali la kujiuliza, mwisho wa mazungumzo yenu anakusaidia nini?

Ndio hatukatai kuwa katika group la marafiki huwa kuna story za aina mbalimbali lakini si vema kuongea mambo ya ndani ya kwako na mwenza wako kwa rafiki kwasababu dunia ya sasa kumpata rafiki wa kweli ni vigumu sana tena sana.

Naongea hivyo kutokana na baadhi ya suhuda nyingi ambazo nimekuwa nikikutana nazo kutoka kwa watu tofauti tofauti, kuwa marafiki wamekuwa ni chanzo kikubwa cha mahusiano kuvunjika ama kwa kutengeneza uongo kutoka pande moja kwenda pande nyingine, au kwa kumchukua kabisa mpenzi wa mwenzake na hii inategemea na mazingira au msimamo mliojiwekea nyinyi wapenzi.
Kuna baadhi ya mahusiano huwa yanakuwa imara sana kutokana na misimamo ya wahusika, mtu huwezi kusikia jambo linalomhusu mwenzi wako halafu ukachukua hatua moja kwa moja au kununa au kupoteza kabisa mawasiliano.

Mtafute umuulize au chunguza kwanza. Nimewahi kushuhudia rafiki wa karibu akijaribu kuharibu penzi la rafiki yake eti tu kwa sababu anaona anapata mafanikio au kwa sababu nyingine ambazo anazijua yeye. Anataka amtafute mtu wa pembeni, ampe namba ya mpenzi wa rafiki yake halafu amtukane na amwambie aachane na rafiki mtu.
Hivi hii yote ili iweje? Sana sana unakuwa unajishusha. Naamini siku zote wivu unaotakiwa ni ule wa maendeleo lakini siku hizi marafiki wana vitu vya ajabu ajabu huo unaitwa urafiki wa KICHINA.
Fanya mambo yako wewe kama wewe marafiki ndio wapo, lakini sio wa kuongea nao kitu chochote kuhusu mahusiano yako au hata matarajio ya maendeleo yako wengine wakiona unafaidi/unafanikiwa sana wanaweza kufanya njia yoyote kukufunga hata kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa wenye imani hizo ili tu uharibikiwe hiyo ndo furaha yao.

KUWA MAKINI NA MARAFIKI HASA KWENYE MAHUSIANO.
Si lazima umshirikishe katika kila jambo, siku hizi marafiki wa kweli ni wachache sana...