Juventus yaicharanga 3-0 napoli

ROME (AP)-Juventus imewapiga Napoli 3-0 Jumapili hii na  kusonga kwa pointi mbili dhidi ya AC Milan iliyokuwa inaongoza katika ligi hiyo na kuanzisha vita ya vuta nikuvute ya nani atachukua ubingwa.katika raundi iliyobaki

Leonardo Bonucci alifunga bao la kwanza katika dakika ya 53 kwenye Uwanja wa Juventus, Arturo Vidal aliongeza bao lingine dakika ya 75, na Fabio Quagliarella kumaliza katika dk ya 83.Juventus ilitawala mchezo mwanzo hadi mwisho wa mchezo kuhakikisha wanajiwekea mazingira ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo

Comments