Lionel Messi alifunga penalti mbili katika kipindi
cha kwanza na kusaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AC
Milan.
Kwa ushindi huo katika mechi iliyochezwa uwanja
wa Nou Camp sasa Barcelona wamefuzu kwa nusu fainali ya kombe la klabu
bingwa barani Ulaya kwa mwaka wa tano mfululizo.Mabao hayo ya Messi katika mkondo wa pili wa mechi ya robo fainali yamemfanya kuwa na jumla ya mabao 51 katika michuano ya ligi ya mabingwa na akiwa na umri wa miaka 24.
Hii inamfanya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kabisa kupita wote kufikia nusu karne ya mabao na pia kuvunja rekodi ya kufunga jumla ya mabao 14 kupita rekodi yake aliyeshikilia pamoja Ruud van Nistelrooy ya kufunga jumla ya mabao 12 katika msimu mmoja.
Bao la Andres Iniesta katika nusu ya pili lilikamilisha ushindi wa Barcelona ambayo katika nusu fainali watakabiliana na mshindi wa pambano kati ya Chelsea na Benfica.
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!