POLISI WAHAMISHIA MAKAZI UBUNGO

ffu wakiwa tayari kwa lolote
polisi wakilinda usalama eneo la ubungo dhidi ya machinga
Kufuatia kauli iliyotolewa na Tanroads pamoja na Tanesco ya kuwataka wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa wanafanyia biashara zao katika meneo ya kando ya barabara ya ubungo pembezoni mwa uzio wa mitambo ya umeme wa tanesco jijini Dar es salaam.Imewalazimu polisi kutumia nguvu kuwaondoa wafanyabiashara hao.kwani wengi wao walikuwa wabishi mapaka pale polisi walipowatishia kwa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi ndio wakaondoka na kutishia kuwa watarudi tena kuendlea kufanya biashara zao maeneo hayo. Hali hiyo imewafanya polisi wa kutuliza ghasia kusambaa maeneo hayo siku mbili hizi,ili kuhakikisha raia hao hawarudi kufanya biashara hapo.hata hivyo hali hiyo imesaidia sana kuondoa msongamano wa watu uliokuwepo mwanzoni kabisa.sasa hali ni shwari watu wanapita kwa kujinafasi tu.

Serikali imewataka machinga hao kuhamia katika soko lao liliopo ilala jijini dar.maeneo mengine ambayo hayaruhusiwi ni mwenge.
machinga wakilalamiki auamuzi wa kuwaondoa hapo ubungo

Comments