NIMEKUTANA NA MICHAEL JACKSON JEHANAMU YA MOTO -BINTI ATOA USHUHUDA.SOMA HAPA SEHEMU YA 02


 Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona Mbingu na kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.” Haikuwa rahisi niliposikia neno hili.
4
"Nitakufa namna gani? mie mdogo sana", Nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote, Kila kitu Mungu afanyacho hakina makosa wala mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya Mbinguni na Kuzimu, kwakuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema “Amen, lakini nitagongwa na gari au nitakufaje?” Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana akaniambia nisihofu, kila kitu kiko katika uwezo wake. Nikasema, “Ahsante Bwana”
Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao walikuwa hawaongei nami; bali walidumu kusema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa Mbinguni. Roho Mtakatifu pia alikuwa na malaika wale huku akifurahi. Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka kwa mwovu ili kuwafanya watu wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua injili haikeri wala kuchosha, niburudisho la ajabu hapa duniani!
Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho Mtakatifu. Lakini malaika walikuwa hawaongei nami, ila walikuwa wakimsifu Bwana. Nikimwambia Roho twende nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami. Ninaweza kujihisi na kumwona vema.

Japokuwa wengi hawamwoni, yeye yupo! Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha yake na faida za Roho Mtakatifu…… hakuna njia ya kujitenga naye jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi!
Tarehe 7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema “Jiandae, kwakuwa leo utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile nilimwona vema. Niliipuuza sauti yake na kusema “Bwana, Sitaki kufa leo!” Lakini alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!” Mara hii sauti ilikuwa ya juu zaidi na mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke. Nitafanya kila utakalo niambia, najiachia kwako Bwana, japo naogopa, najua upo nami, nawe ni wa kweli.” Niliomba, “Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia kunipa ujumbe mara ya kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani, na umpe tena neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa mara zote Bwana hujua ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo nilipofika nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona mtumishi wa Bwana, akasema, “Bwana akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je uko tayari? Kwa kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica alisimama na kushikwa na mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya vilevile alivyomwomba njiani.
Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa, sitakufa! Hapana, Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Ameni" na tukaomba. Ghafla nikajisia hofu yote imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko vyote nikitamanicho kinifike! Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo kila mmoja
5
aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge na kuwa mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
Picha wakimwombea:
Maxima:
Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu
kilichokuwepo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”
Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni, unafuraha
na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye,
lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote wakastaajabu na
kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama kwa
mshangao zaidi!
Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”ITAENDELEA JUMATATU IJAYO

USIKOSE MPENZI MSOMAJI NA MUNGU AKUBARIKI........