Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa miaka 18, na ninasoma chuo cha
"Colegio José María Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador. Kwanza nilimpokea Kristo nilipokuwa na umri wa miaka
12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata mmoja wa rakifi zangu aliyeokoka na nikajisikia
aibu miongoni mwao", kwa hiyo nirudi nyuma mbali na Mungu na kuishi maisha mabaya. Lakini
Mungu alinivuta nitoke huko.
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 15, nirejea tena kupatana na Bwana, lakini nia haikutulia sawa
sawa. Biblia inasema (Yakobo 1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika nia zake zote" na mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu. Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo vizuri, ni
vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo, nataka kuwa hivyo, hakuna mtu wa
kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala chakufanya, wala namna ya kuvaa, au mwenendo."
Naye alijibu, "Mungu atakushughulikia na atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17, nilimkaribia Bwana. Tarehe 28 mwezi Aprili nilimwendea
Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi” na
nilimweleza jinsi ninavyojisikia. "Bwana, nisamehe mimi. Natamani uandike jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee niwe mwanao." Nilitubu na kutoa maisha yangu kwa Bwana rasmi.
Nikasema “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti ndani mwangu." Nililia kwa moyo wangu
wote, huku nikimwomba Bwana anibadilishe mimi. Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita,
sikuona madiliko yoyote. Badiliko pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma biblia na
kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha yangu.

Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa katika mfungo wa siku 15. Niliamua kushiriki, lakini kabla
ya kuanza nilisema: “Bwana, naomba unishughulikie hapa." Katika kipindi chote cha mfungo,
Bwana alikuwa anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana hajaniona,
na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia mimi?" Nikaomba na kulia peke
yangu na kusema tena, "Bwana, je unanipenda? Je upo hapa? Upo nami hapa? Kwanini husemi
nami kama unavyosema na kila mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata maneno
ya unabii, lakini siyo kwangu" Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana akanipa neno la
Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu
usiyoyajua." Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu nilisikia sauti yake na kupata
maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia 33:3.
Nikasema “Bwana, hiyo ni kwaajili yangu?” Nilitunza na kukaa nalo kimya mwenyewe wakati kila
mmoja akishuhudia waliyopewa na Bwana na kuoneshwa. Lakini mimi nilitunza siri yangu na mara
kwa mara nilijikumbusha na kutafakari maneno: " Niite" maana yake nimwombe, lakini nini maana
ya: "mambo makubwa, magumu" niliwaza, “Huenda ikamaanisha Mbinguni na Kuzimu." Kwahiyo nalimwambia “Bwana, naomba unioneshe Mbinguni tu, lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kuzimu ni sehemu ya kutisha na mbaya sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo wangu wote, "Bwana kama ni mapenzi yako kunionesha, na iwe hivyo, lakini nibadilishe kwanza. Naomba ufanye tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti.”
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na vipindi vigumu na mara nyingine nalijisikia kuishiwa nguvu, siwezi tena kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu. Nilianza kusikia sauti yake na kumjua vema zaidi. Tukawa marakifi wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu pia. Niliwahi mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka kukujua vema," na nilishirikiana naye katika mawazo yangu yote.
Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja nyumbani kwetu na kusema, "Bwana akubariki." Nikajibu, "Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja kukuletea ujumbe toka kwa Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana atakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa unamwomba neno la Yeremia 33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini umepataje kujua? Sijamweleza yeyote." Akanijibu, "Mungu unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila kitu."
Mara tukaanza kuomba. Baadhi akina dada toka kanisani kwetu na wana familia wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona Mbingu zikifunguka. Mara nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili wanashuka kuja tulipo" Mtumishi wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja hapa”
Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye kung’aa, na walionekana wakiangaaza, mng’ao kama wa dhahabu. Walivaa sandozi za vito vya thamani na walivaa mavazi matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo hapa kwasababu tuna kazi yakufanya….. tupo hapa kwasababu unatakiwa utembelee Mbinguni na kuzimu na hatutaondoka mpaka yote yatakapo pita." Nikawajibu “safi sana, lakini mimi natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu” Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote zaidi. Baada ya kumaliza maombi, niliendelea kuwaona wakiwepo.
Pia nilianza kumwona Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na yuko kila mahali wakati wote. Ninamwona, anaangaza na kung’aa sana, naona tabasamu lake na mtazamo wake wa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni mzuri zaidi ya malaika. Malaika wana uzuri wao lakini Roho Mtakatifu ni zaidi sana kwa yote. Naweza kuisikia sauti yake, sauti ilijaa upendo na matulizo makuu. Siwezi kuelezea kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo huo yakuvutia. Yeye husema “Niko pamoja nawe” Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea kutembea na Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira. Tulikuwa tunapita kipindi kigumu sana, lakini chenye ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa shule na pia darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona Mbingu na kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.” Haikuwa rahisi niliposikia neno hili.
ITAENDELEAA......JUMATATO IJAYO