MSANII LAMECK DITTO ATEMBEA KWA MGUU KUTOKA TABATA MPAKA KIGAMBONI!!! MSIKILIZE MWENYEWE HAPA



Lameck Ditto ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo hivi leo. Bila shaka tunakubaliana kwamba Ditto  ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye vipaji, nidhamu na juhudi za hali ya juu katika sanaa ya muziki.
Kufikia hapo alipo, alipitia mengi. Alistahimili mengi. Aliwahi kuambiwa hawezi. Aliwahi kutembea kwa mguu masafa marefu ili kwenda studio kwa sababu mfukoni hakuwa na nauli hata ya daladala. Kukaja masuala binafsi ya kufiwa na Mama yake mzazi akiwa bado kijana mdogo tu. Kwa muda mrefu hakumjua baba yake. Akaishi kwa kubahatisha kama vile mtoto wa mtaani. Pamoja na yote hayo,akaendelea kuamini kwamba anaweza na sanaa ndio itakayomtoa. Kama alivyoimba katika wimbo wake “Tushukuru Kwa Yote”, Ditto akaendelea kushukuru na sasa anaanza kuonja mafanikio ya uvumilivu;

MSIKILZE HAPA CHINI AKIELEZEA  MKASA WA KUTEMBEA MASAFA MAREFU PAMOJA NA WIMBO AUPENDAO


0 comments: