UPANDE wa serikali katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkbaili
msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye
anadaiwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba, jana
ulimsomea kwa mapana kesi inayomkabili mshtakiwa huo (Comittal
Procedings).
Wakili Mwandamizi wa Serikali Shadrack Kimaro mbele ya Hakimu
Mkazi Mmbando alidai kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kumsomea
maelezo ya awali mshtakiwa huyo na alianza kwa kumsomea maelezo uya
mashahidi ambao anakusudia kuwaleta katika kesi hiyo na maelezo ya
onyo ya mshtakiwa huyo pamoja na kuvitaja vielelezo watakavyovitumia
katika kesi hiyo hiyo itaakapoanza kusikilizwa Mahakama Kuu.
Wakili Kimaro alieleza kuwa pia wataleta mashahidi tisa na
vielezo ikiwemo ramani ya eneo la tukio kwenye chumba alichofia
marehemu Kanumba, ripoti ya uchunguzi wa kifo na maelezo ya onyo ya
Lulu.
Aliwataja mashahidi hao wanaokusudia kuwaleta katika kesi hiyo ni
Sethi Kamugisha (24) ambaye alikuwa akiishi na Kanumba, Sophia Kassim
(45) ambaye alimpangisha Kanumba, Dk Paplas Kagaiga (29) ambaye alikuwa
daktari wa Kanumba, Esther Zefania (40) askari polisi Oysterbay, Morris
Sefwao mkazi wa Kijitonyama, Mrakibu wa Polisi (ASP) Daniel Shilla
kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Kinondoni, Dk Magreth Ibobo
(40) ambaye aliombwa na familia ya Kanumba kusimamia upasuaji wa mwili,
Inspekta Mwesiga (35) Afisa Uhamiaji kutoka kituo cha Horohoro Tanga na
Ditective Sajent Renatus wa kituo cha polisi Oyesterbay.
Akisoma maelezo ya onyo ya Lulu mbele ya Hakimu Mkazi Augustina
Mmbando, wakili wa serikali, Shadrack Kimaro, alidai kuwa Lulu alitoa
maelezo hayo Aprili 7 mwaka huu katika kituo cha polisi Oysterbay mbele
ya askari wa kituo hicho Ditektive Sajent Renatus.
Alidai kuwa Lulu alizaliwa mwaka 1994 na kwamba alimaliza kidato
cha nne katika shule ya Sekondari ya Midway na baada ya hapo aliendelea
na shughuli za sanaa ambazo aliianzia kuzifanya tangu mwaka 2000.
Kimaro alidai Lulu alifahamiana na Kanumba kwa muda wa miaka 10 na
walikuwa wakifanyakazi za sanaa ya uigizaji pamoja na Januari mwaka huu
ndipo walipoanza rasmi mahusiano ya kimapenzi.Katika mahusiano yao ya
kimapenzi hawakuwahi kuishi pamoja isipokuwa alikuwa akienda nyumbani
kwa marehemu anapojisikia na alikuwa wakati mwingine akilala huko.
Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi cha miezi minne ya mahusiano
yao walikuwa wakigombana mara chache lakini sababu kubwa ilikuwa ni
wivu wa mapenzi kwa sababu wote walikuwa hawaaminiani katika mahusiano..
Pia wakili huyo alidai kuwa Aprili 5 mwaka huu Kanumba na Lulu
walitumiana ujumbe mfupi wa simu. Baadhi ya jumbe hizo zilisomeka hivi.
Kanumba: Uniheshimu, unanidharau, unanijibu unavyotaka wewe..
nakupenda sana..this love kill me soon..vipi baby mzima umekula?
nakupenda mke wangu..natarajia kwenda USA hivi karibuni je nikuletee
zawadi ipi kwa ajili ya birthday yako?
Alidai kuwa Lulu alimjibu kwa kumtumia ujumbe wa kumtuliza kama
vile nakupenda mme wangu..niletee zawadi yoyote ile lakini ujumbe
mwingine haukumbuki na kwamba walipatana siku hiyo hiyo.
Alidai kuwa jioni ya siku hiyo Lulu alimpigia simu Kanumba na baada
ya muda mfupi alikwenda nyumbani kwake Sinza Vatican. Alidai kuwa
alipofika kwa Kanumba chumbani kwake alimkuta akinywa pombe ambayo
ilikuwa imechanganywa na soda na ghafla simu yake iliita na alipotoka
nje kutaka kwenda kuisikiliza Kanumba alimfukuza hadi barabarani.
Alidai kuwa baada ya kumkimbiza alimkamata na kuanza kumpiga vibao
na mateke huku akilalamika kwamba anamdharau na alimpeleka hadi
chumbani ambapo alichukua panga lililokuwa chini ya kitanda na kuanza
kumpiga kwa ubapa.
Alidai kuwa baada ya kumpiga kwa upanga ghafla alitupa panga
chini huku akiwa amesimama alianza kupumua kwa taabu na baada ya muda
mfupi alipojigonga ukutani na kuanguka chini. Alidai baada ya kuanguka,
Lulu alikimbia na kwenda kujifungia chooni kwa hofu na baada ya muda
alitoka na maji na kwenda kummwagia Kanumba lakini hakuamka.
Alidai kuwa baada ya kuona hali hiyo alishikwa na hofu na kuamua
kukimbia kwenye ufukwe wa Coco Beach.Alidai kuwa akiwa huko alipewa
taarifa kuwa Kanumba amefariki na ndipo alipompigia simu rafiki yake ili
aende kumsaidia kuendesha gari waelekee kwenye msiba.
Kwa mujibu wa maelezo ya mashahidi yaliyosomwa mahakamani hapo
inadaiwa kuwa Aprili 6 mwaka huu saaa 3 usiku Kanumba akiwa nyumbani
kwake, alimwambia mdogo wake Sethi asitoke kwakuwa kuna mahali wanataka
kwenda hivyo amsindikize na kwamba alikuwa akinywa kinywaji aina ya
Wisky.
Inadaiwa kuwa ilipofika majira ya saa 6 usiku Lulu alifika nyumbani
kwa Kanumba na kuingia hadi chumbani na baada ya muda walianza
kugombana na baada ya kuanguka mapovu yalianza kumtoka mdomoni.
Aidha alileza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, mdogo wake
aliwasiliana na daktari wa Kanumba na baada ya kufika aligundua kuwa
Kanumba tayari alikuwa amefariki lakini alishauri apelekwe hospitali
ndipo walipoamua kumpeleka hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baada ya
kupimwa iligundulika kuwa amefariki.
Na baada ya Kanumba kufariki, Lulu alitoroka na baada ya kutafutwa
aliwekewa mtego na kukamatwa saa 11 alfajiri katika eneo la Bamaga na
kupelekwa kituoni Oysterbay.Uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kuwa
hakukuwa na jeraha lolote kuanzia kichwani hadi mwilini.
Baada ya kusomwa maelezo hayo Hakimu Mmbando alimuhoji Lulu kama
ana lolote la kuongea na baada ya kujadiliana na wakili wake, Lulu
alijibu kuwa ana cha kuongea.
“Mahakama hii inaziarifu pande zote
mbili katika kesi hii kuwa kesi yenu leo imefikia mwisho katika mahakama
hii hivyo jarada la kesi hii linaamishiwa mahakama kuu tayari
kwaajili ya kuanza kusikiliza na kwamba Lulu utaendelea kuishi
rumande hadi pale utakapokea wito toka Mahakama Kuu wa kukuita kwaajili
ya kesi yako.”alisema Hakimu Mmbando na kuahirisha kesi hiyo.
Wakati huo huo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana
isikiliza ombi la kuomba apatiwe dhamana Mwenyekiti wa Mpira wa Soka
mkoa wa Pwani(COREFA),Hussein Othman Hussein ‘Hassanor’ na wenzake sita
wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya Sh bilioni 1.1 ambapo
wanadaiwa walisafirisha kontena na pembe za ndovu kinyume cha sheria
kutoka Tanzania kwenda Hong Kong nchini China.
Jaji Zaina Mruke alisikiliza ombi hilo ambapo Hassanor alikuwa
akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Richard RWeyongeza ambao upande
wa Jamhuri ulikuwa ukiwakiliwa na mawakili wa serikali waandamizi
Biswalo Mganga, Mutalwemwa Kishenyi, Benard Ikokola ambapo hata hivyo
mawakili wa serikali waliomba Hassanor asipewe dhamana kwasababu
ametenda kosa la kesi hii wakati tayari anakabiliwa na kesi ya awali
Na.209/2011 iliyopo mahakama ya KIsutu mbele ya Hakimu Devota Kisoka ,na
kisheria mtu yoyote anayetenda kosa wakati yupo ndani ya dhamana
,mshtakiwa huyo anatakiwa asipewe dhamana.
Jaji Mruke aliarisha kesi hiyo jana saa 12:20 jioni hadi jumatatu saa
tatu asubuhi ambapo atakuja kutoa uamuzi wa ama ampatie dhamana
Hassanor na wenzake au laa.
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!