Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani mwenye fulana ya mistari akiwaonesha waandishi wa habari Cds za video na Audio za Muziki wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limeendesha Operesheni maalum ya kukamata maharamia wa kazi za wasanii nchini na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 25 wakiwa na mashine za kurudufu CD na mali zingine zenye thamani ya zaidi ya Milioni 67.
Kufanyika kwa Opresheni hiyo kunafutia taarifa zilizotolewa na baadhi ya wasanii nchini ikiwemo wa filamu, nyimbo za injili na Bongo fleva kulalamikia kitendo cha baadhi ya wenye maduka ya CD mjini Dodoma kuuza kazi zisizokuwa na hatimiliki zao.
Akizungumzia tukio hilo,
Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, ALEX MSAMA amesema vitendo hivyo vinarudisha nyumba maendeleo ya wasanii kwani licha ya gharama kubwa wanazotumia wamekuwa hawanufaiki na kazi zao.
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!