UREMBO:Jinsi ya kuzifanya nywele zako ziwe ndefu na za kuvutia

Kuwa na nywele ndefu na zinazong'aa ni ndoto ya kila mwanamke na kuzipata nywele dizaiini hiyo imeonekana  ni kazi ngumu sana,.Kuna mwengi wamejaribu kwa muda mrefu lakini wameshindwa kufanikisha kuzipata nywele za wanazotaka.Wakati mwingine, ni kwa sababu ya genes, matatizo ya homoni, ukosefu wa huduma, ukuaji hafifu wa nywele zako nk...

Usiwe na wasi wasi kuhusu hilo kama tatizo lako linahitaji ufumbuzi wa kidaktari.Kwa kufuata yafuatayo unaweza kupata kile ulichokitafuta muda mrefu.pengine ulikuwa hujui  tatizo linalokukabili linasababishwa na nini.


Lazima kufanya mabadiliko katika kiasi cha maji unachokunywa kwa siku. Kunywa angalau glasi 10 za maji kila siku na pamoja na hayo,ongeza glasi angalau 2 za maji ya nazi pia. Hii inaweza kuwa baraka kwani itaweza kufichua au kuchangamsha mfumo wako mzima wa ukuaji wa nywele .
 Pia, matatizo kama ya mba au mgawanyiko mwisho, nywele kuanguka ni vitu unavyotakiwa kuwa navyo makini sana.kwani pia inaweza kuwa vikwazo vikwazo katika ukuaji  wa nywele. Hvyo, unatakiwa kutumia mafuta maalum pamoja na mafuta ya nazi,pia kuosha nywele zako kwa shampoo pale unapojisikia kuosha nywele zako  na kutumia dawa zinaondoa mba
Pia, kuhakikisha kwamba unaongeza ulaji wa vyakula vyenye protini kwa wingi kama  vile mbogamboga za majani, samaki, maziwa, nafaka, mayai, nk katika mlo wako. hii husaidia kuzipa nguvu nywele na kuimarisha mizizi ya nywele zako.Chana nywele zako mara 6 au mara 7 kwa  siku ili kuboresha mzunguko wa damu kichwani



Kama utayafuata hayo basi itasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa nywele zako,USIKOSE MUENDELEZO WA MADA HII HIVI KARIBUNI PIA KAMA UNA LOLOTE UNAWEZA KU COMMENT HAPO CHINI YA POST HII

Comments