RAIS KIKWETE KUWAPA POLE WAJANGA WA AJALI YA MELI ZANZIBAR
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete.amefika nchini zanzibar kwa ajili ya kutoa pole kutokana na ajali ya meli ya MV Skagit iliyopata ajali visiwani Zanzibar, iliyoondoka Bandari ya Dar es Salaam saa 06.05 mchana juzi ikiwa na abiria 248, watoto 31 pamoja na mabaharia 9.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete walitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi na hospitali kuu ya Mnazi Mmoja
![]() |
| meli ya mv skagit ikimalizia kuzama |
Meli hiyo
inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport, ilipata usajili katika
Mamlaka ya usafiri Bandari Zanzibar (ZMA)ikiwa na uzito wa meli
(GRT)96.
Idadi ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni zaidi ya
34, majeruhi 146 wakati wengine wakiendelea kutafutwa.
0 comments:




