ALIKIBA KAMZIDI VITU VINGI SANA DIAMOND SEHEMU YA KWANZA

Kwa muda sasa mashabiki wa muziki nchini wamekuwa wakijenga ubishi mkali kuwa nani msanii mkali kati ya ALLY K au PLATNIUM,kama ambavo wenyewe wanajiita.Tatizo kubwa watu wanajenga hoja bila kuwa na uhakika au kufanya utafiti.Nimeamua kufunguka hapa kwa kupitia kipengele kimoja hadi kingine na wewe msomaji utajua ukweli kama utasoma na kuelewa vizuri.

CHIMBUKO
Kwanza ifahamike kuwa alikiba ameanza kuingia katika gemu hili tangu mwaka 2003 lakiini alikuja kufahamika zaidi mwaka 2004 baada ya kutoa kibao cha sinderela.Lakini diamond ameanza kutambulika kimuziki mwaka 2009 baada ya kutoka na wimbo wake wa kamwambie..Hivyo alikiba ni mkubwa (mkongwe) kwa diamond.

UMRI
Alikiba alizaliwa Iringa Novemba 26, 1986 kutoka kwa mama yake Tombwe Njere na Saleh Omari. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wane katika familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba.Diamond anasema amezaliwa mwaka 1989, lakini chanzo cha kuaminika kinasema, Diamond amezaliwa mwaka 1987 HIVO alikiba ni kaka kwa diamond.

COLLABO ZA NDANI YA NCHI
Kwa kuwa alikiba ameanza kuimba kitambo toka wnzi za njiwa,mpaka sasa ameshafanya kolabo na wasanii wengi sana wa east africa.ukiongelea wasanii 5 wanaoongoza kwa kolabo hapa nchini lazima utamtaja kiba.Alikiba kafanikiwa kuwaleta wasanii wengi sana chipukizi katika gemu na wakafanikiwa kutoka.mfano mzuri ommy dimpoz,tox star n.k   UPANDE wa PILI Diamond ameanza kufanya kollabo na watu hivi karibuni na amefanya kazi na wasanii wachache sana ambao wanahesabika.mfano sheta,ommy,prof jay, na wengine wachache.
COLLABO ZA NJE
Diamond amefanya kolabo na wasanii wengi wa nigeria na east africa kama davido,iyanya n.k .kati ya hao wote hakuna ambaye anakaribia level za R KELLY ambae alimchagua alikiba kufanya nae ile project ya hands aliowashirikisha wasanii wengine wa africa wanaoweza.

itaendelea.kesho 
kuna MAPENZI,HESHIMA,BIFU,UTAJIRI, VYOTE HIVO TUTACHAMBUA