MENAS MBUNDA ANDOYA NYOTA ILIYOZIMA WAKATI BADO TUPO GIZANI sehemu ya kwanza


mzee Menas mbunda Andoya

Hakika; Baada ya dhiki faraja” Msemo huu wa Waswahili sasa una maana kubwa kwa Menas Mbunda Andoya, mzalendo wa Tanzania aliyebuni mradi wa umeme wa maporomoko ya maji takriban miaka 13 iliyopita. Wazo la Mtanzania huyo kuanzisha mradi huo lilimfanya akumbane na vikwazo mbalimbali ikiwamo kufukuzwa kama kuku na watu katika ofisi zao huku akipigwa vita kila kona. 

 Hata hivyo, Andoya ambaye pia alikuwa ni ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Andoya Hydro Electric Power Co. Ltd (AHEPO), hakuchoka wala kukata tamaa, bali aliendelea kuwa jasiri, hatimaye mradi wake mkubwa wa umeme wa maporomoko ya maji alioubuni mwaka 2000 umezaa matunda, badaa ya kufanikiwa kuwasha umeme kwa majaribio. 
 Ungebahatika kuonana naye Andoya(56), anavyofahamika na wengi ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma akiwa ni mtoto wa tatu kati ya saba, akiwa pia mume na baba wa watoto watatu wa kiume na mmoja wa kike. Kitabia ni mcheshi, mwenye busara na mtu anayejiamini. Kwa maelezo yake alisema kuwa alikuwa na hamu kubwa kuona anafanikiwa kuhakikisha siku moja anatimiza ndoto yake na Watanzania wenzake wanapata huduma ya umeme na kufa akiwa na faraja la kutimiza lengo hilo.Na kama alijua vile kwani amefariki dunia akiwa katika harakati za mwishoni kabisa kukamilisha mradi huo
watu wakiwa katika eneo la nyumbani kwa marehemu
 Alisema kuwa madhumuni ya mradi huo ni kuzalisha umeme MW 1 na kuunganishwa kwa wateja wa awali 922 kati ya 3,835 katika Vijiji vya Lifakara, Kilimani na Mbangamao na ziada kuuzwa Tanesco ukilenga kupata umeme kwa njia endelevu na nafuu. Andoya aliweza kukamilisha ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kutoka Mbinga hadi Kituo cha Uzalishaji na usambazaji katika Vijiji vya Lifakara, Kilimani na Mbangamao umekamilka.pia wa ujenzi wa bwawa, mfereji wa maji na nyumba ya mashine yamekamilika na ujenzi utaanza kipindi kifupi kijacho. 

Awali madhumuni yake yalikuwa kutumia nguvu ya maji kuendesha mashine za kukoboa na kusaga nafaka ili kupunguza gharama kwa wananchi wa vijiji vya jirani kwa kutoa huduma hiyo kwa bei nafuu na kuinua maisha yao, ambapo mradi huo ulianza kwa jina la Nguvu ya Maji Partinership. Mwaka 2005 Kampuni ya Andoya Hydroelectric Power Co Ltd ilisajiliwa na upembuzi yakinifu wa mradi ulikamilika, hatimaye taarifa ya upembuzi yakinifu na mchanganuo wa mradi ulipitiwa na wataalamu mbalimbali wa taasisi za Serikali ikiwamo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), NEMC, Ewera na wataalamu kutoka Benki ya Dunia na wote kuafiki kuwa kiasi cha MW 1 kinaweza kupatika katika maporomoko hayo ya Mto Mtandasi. Kufikia Novemba 2012, mradi huo ulifanikiwa kupata vibali na fedha za kutekeleza, ukiwa katika hatua mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa njia ya usafirishaji wa umeme yenye urefu wa kilomita 14 kwa kiwango HT kutoka Kituo cha Umeme cha Mbangamao hadi Makao Mkuu ya Wilaya, ili kuunganisha na gridi ya Tanesco pamoja na Vijiji vya Lifakara (2 km), Kilimani (4 km) na Mbangamao (4 km).
mzee andoya enzi za uhai wake

 Awamu ya pili kuwa ni ujenzi wa njia za kusambaza umeme kwa watejaGharama za ujenzi wa mradi huo ni Sh 4.5 bilioni, ambapo asilimia 30 zilichangwa kutoka mtaji wa Kampuni ya Andoya Hydro Electric Power Co. Ltd (AHEPO), asilimia 70 ni mkopo kutoka Benki ya CRDB, mkopo wa benki ya Dunia kupitia Serikali na taasisi zake ikiwamo (REA) chini ya mpango wa Tanzania Energy Development and Access Project (TEDAP), ambapo pia Unido wameahidi kuchangia Dola 250,000 za Marekani.