Watalaam wa afya nchini Ujerumani wanasema kuwa maradhi
yanayosababishwa na matango ni bakteria wapya, na wanaweza kuathiri
maini na damu ya mtumiaji.
Backteria hao ambao wamezuka huko Ujerumani na Sweden hadi sasa
wamesababisha vifo vya takriban watu 18 na zaidi ya watu 1500
wameathiriwa na backteria hao baada ya kula matango hayo.
Waatam wa kiafya kutoka Shirika la Afya Duniani WHO wanasema kuwa hali
hiyo haijawahi kushudiwa, huku wanasayansi kutoka China wakidai kuwa
bakteria hao ni hatari sana na wana sumu ambayo pia inaweza kusambazwa
kwa haraka.
Aidha, Serikali ya Uhispania imepinga taarifa kutoka Ujerumani, inayodai kuwa matangao hayo, yametoka nchini humo.
Bakteria hao wamesababisha idadi kubwa ya watu kuharisha nchini Ujerumani na wataalam wa kiafya wameonya wasafiri wanaoelekea Ujerumani, kutokula matango hayo kwani yanaweza hatarisha usalama wa maisha yao.