Utafiti kuhusu imani ya watu wanaoishi katika nchini 137 ambao
umetengeneza kitabu chake kipya, umegundua kuwa upagani unazidi
kuongezeka zaidi kwenye nchi zilizoendelea kutokana na utajiri.
Utafiti huo umeelezea pia imani maarufu kuwa watu wenye dini
watawatawala wapagani kwakuwa wao (watu wa dini) huzaa watoto wengi.
Dr Nigel Barber amekiita kitabu chake, ‘Why atheism will replace religion,’ (Kwanini upagani utachukua nafasi ya dini).
Amesema wapagani wengi wapo kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi na dini
itapungua kwa watu kutokana na kuongezeka kwa utajiri wa mtu mmoja
mmoja.