HIZI NDIO PICHA ZA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA IFM KWA KAMANDA KOVA!!! @9photoss
Kufuatia wimbi la majambazi kuwasumbua na kuwafanyia vitendo vibaya
ikiwemo kubakwa kwa wanachuo hao,wameamua kuandamana mpaka katika ofisi
za makao makuu ya polisi na kutaka kuongea na Kamanda wa Polisi wa Kanda
maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova ili atoe
tamko kwanini ombi lao la kuomba ulinzi katika hostel zao hizo zilizopo
kigamboni kutofanyiwa kazi na matokeo yake kila siku wanazidi kufanyiwa
vitendo vya kinyama na majambazi.
Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili
wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo
ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa hali
iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai
kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo
vya kulawiti.
0 comments: