mikosi yazidi kumuandama Lindsay Lohan

Ikiwa bado ana ONYO la kuwa raia mwema muigizaji lindsay lohan amekumbwa na balaa jingine baada ya kumgonga na gari meneja wa club mmoja ya burudani hivi juzi.
  Imeripotiwa kwamba wakati akitoka katika club maarufu ya  Sayers Club mjini Hollywood jumanne usiku alimsababishia maumivu ya mguu meneja wa club hiyo baada ya kumgonga kwa bahati mbaya na gari yake aina ya  Porsche wakati akiwa anageuza gari hilo kwa ajili ya kuondoka.

Baaada ya tukio hilo ni kuwa lindsay aliondoa gari kwa spidi kali kitu alichokuja kusema baadaye kwamba aliogopa mapaparazi,Mwanzoni polisi walipopigiwa simu walipuuzia ishu hiyo kwa kuwa ilidaiwa meneja huyo hakupata jeraha lolote lakini  kesho yake  mapema meneja huyo alipoanza kuhisi maumivu ya mguu na kwenda kupata matibabu haraka na habari zaidi zinasema kwa meneja huyo kwa sasa ana ana mpango wa kudai fidia kwa muigizaji huyo.
Hivi karibuni lindsay amekuwa ni story katika vyombo mbalimbali vya habari kutokana na matukio yanayomtokea.

Comments