MASHAIRI YA MAPENZI

JE UNAWEZA KUTUNGA MASHAIRI??? NA JE UNGEPENDA KUSHARE NA WENZAKO HAHAHAHAH WAKATI NDIO HUU TUMA SHAIRI LAKO KUPITIA nasmiletz@gmail.com NA TUTALIWEKA HAPA 


  1. Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
    Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
    Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi.
  2. Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
    Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
    Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi.
  3. Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
    Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
    Akili yake ya nyani, aruka inagongana.
  4. Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
    Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
    Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha.
  5. Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
    Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
    Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.
Hashil S. Hashil



Kitu na boksiNachukua wasaa huu, kukupa kitu na boksi
Yasikie yangu makuu, yaliyomo ndani ya boksi
Ni hiari yako mkuu,sitaki kukuletea ubosi
Usitende usiseme suu, usifikiri utaumiza utosi
Weka miguu juu, fungua uone ndani ya boksi

Ni kitu kipya, hakikuguswa na mtu
Si mtumba, wala hakina kutu
Chang'ara, meremeta, chavutia kama sumaku
Hata kabla hujafungua, chanukia kama karafuu
Marashi ya Pemba, na iriki za Tukuyu
Hata kama mbali chatoka, huko Ughaibu
Sitaki  kujidai, na sio majigambo
Kuwa napata kitu na boksi, toka ng'ambo
Ila napiga mahisabati, na kufumbua mafumbo
Jinsi MOLA alivyo nibariki, kwa mengi mambo
Sio tu kiuchumi, Afya na majengo
Pia ndugu, marafiki, na jamaa wa kambo
Hunipatia zawadi, mpya kwa boksi kimtindo
Mpaka langu jipya gari, latoka chumba cha maonyesho

Yote kenda kumi, ni baraka ilioje
Kumpata mwandani, mpenzi mpendanae
Toka kwa MOLA zawadi, wako wa pekee
Lako uaridi, hauchangii na nyuki wala wapambe
Bila shaka ya virusi, gono, wala kaswende
Kama kitu na boksi, fungua uone!!
Mashairi na Subira Mapugilo

Comments