MASWALI MAGUMU YA WANAWAKE KWA WANAUME (MAPENZI)

Wanawake ni watu wenye utambuzi wa hali ya juu sana kwenye swala zima la mapenzi. Unaweza kusema neno moja tu na kupitia neno hilo wakajua kwa usahihi kabisa kwamba wewe ni mtu wa aina gani. Kuna jambo moja ambalo huwa wanaume hawalijui. Ni kwamba pale unapomdanganya mwanamke wakati unapomtongoza na ukampata, si kwamba umempata kwa sababu ya uongo wako, bali ni kwa sababu mwanamke huyo amekupenda, vinginevyo wala usingempata.

1.Unauonaje uhusiano wetu?
Kama jibu lako la haraka haraka litakuwa ni kutarajia kufunga ndoa na kuzaa watoto nk…… Unaweza kumpoteza huyu mwandani wako, kwani kwake yeye atakuona kama unataka kumgeuza mashine ya kutotolea watoto na si vinginevyo. Jibu kama, “nina furaha sana kuwa nawe na sioni kama kuna jambo litakalotutengenisha kati yangu na wewe, huwa najisikia fahari kuwa karibu nawe na nina mararajio makubwa juu yako iwapo mambo yataenda vizuri…” kauli hii inapopenya katika masikio ya mwanamke inamfanya ajisikie fahari sana na ajione kama vile amelamba dume.

2.Ninaonekanaje na nguo hizi nilizovaa?
Mwanamke anapouliza swali la aina hii, anatarajia mwanaume atoe maoni yake si kwa vazi alilovaa kiujumla bali pia anataka kujua maoni ya mwanaume juu kitu fulani kuhusu vazi hilo. Wanawake wangependa kusikia kuhusu rangi ya vazi hilo kama limeendana na ngozi yake ya mwili au aina ya mtindo alioshona kama unamfanya awe na mwonekano gani kulingana na umbo lake.. Je vazi hilo limem-shape vyema nk. Kama ukipatia namna ya kumsifia kulingana na jinsi alivyopendeza lakini bila kutia chumvi utakuwa katika nafasi nzuri ya kudumisha uhusiano. Wanawake ni wajanja sana, iwapo utamsifia kwa kutia chumvi atakusitukia na kukuoana mzushi..

3.Je hutojali iwapo nikikuomba unisaidie?
Jibu kwa swali hilo ni “Sitojali.” Na haraka sana unatoa msaada hata kama hujapenda kutoa msaada huo, wanawake wanapoomba msaada kwa wapenzi wao hawataraji jibu la hapana au vijisababu vya kutaka kuhalalisha kutotoa msaada. Kwa kawaida wanaume ni waungwana sana wanapoombwa msaada na si kwa mpenzi wake tu, bali mwanamke yeyote yule. Kwa kawaida mwanaume anakuwa mwepesi kutoa msaada, hata kama sio wa moja kwa moja, lakini hata mawazo yatakayosaidia kupatikana suluhu ya kile mwanamke alichotaka kusaidiwa. Mwanamke atashangaa sana kusikia jibu la hapana kutoka kwa mpenzi wake na jibu hilo litamfanya amuone mpenzi wake kama mtu asiyejali...


4.Je unawaonaje marafiki zangu?
Kuna msemo mmoja unasema, “unaweza kumjua mtu kutokana na marafiki zake waliomzunguka.” Mwanamke anapouliza swali kama hilo hawatarajii jibu moja tu. Kwa mfano jibu kama, “ni wazuri,” au “ni wachakaramu sana.” Jibu hilo haliwezi kumridhisha mwanamke hata kidogo. Iwapo utawaponda marafiki zake hilo litakuwa ni kosa kubwa, kwani kama utawakosoa kama vile wana tabia zisizofaa, basi atahisi kuwa na yeye umemweka kwenye kundi la wanawake wenye tabia zisizofaa…. Kwa hiyo mwanamke anapokuuliza kama unawaonaje marafiki zake anatarajia ueleze kwa undani jinsi unavyowaona hao marafiki zake, kwa kufanya hivyo atajua kwamba unampenda na kumjali. Sifa za ziada kuhusu huyo mpenzi wako na mmoja wa marafiki zake zinaweza kumfanya mpenzi wako ajisikie vizuri. “Wewe na lara 1 mnavutia sana mkiwa pamoja, maana kila nikiwakuta mko pamoja mnakuwa ni watu wenye furaha wakati wote, huku mkitaniana na kluongea kwa bashasha. Inaonyesha ni kiasi gani mnapendana sana na mnaosaidiana kwa hali na mali….” Unaweza kutoa maoni ya aina hiyo.

5.Vipi, mwishoni mwa juma hili utakuwa na shughuli gani?
Iwe una shughuli au huna, wanawake huwa hawapendi kuwekwa roho juu, linapokuja swala la miadi. Iwapo utamwahidi kuwa mtakuwa na mtoko, basi hakikisha kweli mnatoka na kwa muda mliopanga. Utafanya kosa kubwa iwapo utamwahidi mpenzi wako kwamba mtatoka halafu usitokee….. swala la miadi huwa linapewa uzito mkubwa na wanawake. Iwapo mwanaume atakuwa na kauli kama, “nitaangalia,” au “labda tutapanga kuwa na mtoko juma lijalo.” Kauli za namna hii huwa wanawake hawazipend. Ni vyema mwanaume akawa na uhakika wa kile anachomwahidi mpenzi wake, kama hana uhakika na ratiba yake ni vyema asiahidi. Kama yuko bize yuko bize tu, ya nini kubahatisha. Wanawake wengi huwa hawapendi tabia ya kukurupushwa.

6.Je mpenzi wako wa zamani alikuwaje?
Hili ni swali la mtego kwa sababu kama utamzungumzia mpenzi wako wa zamani kwa namna ya kuonyesha kuwa unam-miss, basi mpenzi wako wa sasa atakuona kama vile bado unampenda mpenzi wako wa zamani, kama utamzungumzia kwa namna ya kuonyesha chuki kupita kiasi dhidi yake, mpenzi wako wa sasa pia atakuona kama vile bado unampenda mpenzi wako wa zamani na unajutia mkitendo cha kuachana naye. Jaribu kutoonyesha hisia za aina yoyote kuhusu huyo mpenzi wako. Zungumzia sifa za jumla za huyo mwenzi wako wa zamani, unaweza kusema kwa mfano “alikuwa ni mtu wa kujichanganya. Pia alikuwa ni mtu mwenye bidii sana tulipokuwa chuoni.” Zungumzia sifa za kile alichokuwa anakimudu zaidi na si kutoa maoni……

7.Je unadhani wazazi wako wananionaje?
Mwanamke yeyote unapompeleka kwa wazazi wako, anakuwa na hisia kwamba yeye sio wa kwanza kupelekwa hapo nyumbani kwa wazazi wako. Yeye atachukulia kama hiyo ni moja ya mchakato wa kufanyiwa tathmini na wazazi wako, ikiwa ni mwendelezo wa wapenzi wako wa zamani uliokwishawapeleka hapo. Anajua kwamba wazazi wako watakuwa wanajaribu kumlinganisha na wapenzi wako wa zamani uliowahi kuwapeleka hapo. Hatopenda kusikia sifa za jumla kutoka kwa wazazi wako, kwa mfano sifa kama, “ni mzuri,” au “anakufaa.” Zitamfanya aone dhahiri kama wazazi wako hawakumchunguza vya kutosha na kuona sifa zake nyingine. Binafsi atadhani kwamba hakupewa uzito unaostahili kuwafunika wapenzi wako wa zamani uliowapeleka hapo kwa wazazi wako. Iwapo wazazi wako watazungumzia sifa za mpenzi wako za ndani kabisa, basi mweleze usimfiche. “mama yangu amekusifu sana anasema una utaalam mkubwa wa mapishi.” Au “Baba yangu amevutiwa sana na uwezo wako wa kujua siasa, hususan wakati ule mlipokuwa mkijadili kuhusu mabadiliko ya katiba.” Unaweza kumwambia……

8.Je unawaza nini?
Wakati mwanamke anapokuwa kimya, ni kwa sababu anawaza kuhusu jambo fulani muhimu. Inaweza kuwa ni namna gani anaweza kusuluhisha ugomvi wake na mmoja wa rafiki zake au ni namna gani anaweza kuendeleza kipaji chake. Iwapo utakuwa unawaza jambo fulani, kiasi cha kukufanya kuwa kimya kwa muda wakati mko pamoja, halafu akakuuliza swali kama hilo na wewe ukamjibu kwamba, unawaza namna ya kurekebisha bomba la maji la chooni lililovunjika. Jibu kama hili litamfanya mwanamke akuone kama vile umechoka kampani yake. Yaani pamoja na kuwa naye karibu lakini unawaza vitu vidogo kama hivyo! Hii kwake yeye atadhani kama hujali uwepo wake. Iwapo utajikuta uko kwenye mawazo mazito ukiwa na mpenzi wako, kisha akakuuliza swali kama hilo, unaweza kumjibu tu kwa kifupi, “Siwazi kitu mpenzi, nina furaha kuwa nawe karibu.” Unaweza kumalizia kwa busu moja matata… hapo utakuwa umemaliza.

9.Je ilikuwaje mpaka ukanipenda?
Swali hili ni gumu sana tofauti na jinsi wanaume wengi wanavyodhani. Hakuna mwanaume anayeweza kumuelezea mwanamke sababu ya kumpenda kwa namna ambavyo yeye (Mwanamke) angependa kuelezewa…. Lakini ili uweze kuepuka mtego huo, unaweza kumjibu kwa kumwambia hivi… “Tangu nikufahamu umenifanya nijiamini, unanifanya nijihisi niko salama na umenifanya nijione napendwa….” Majibu ya aina hii, yatamvutia mwanamke yeyote…

10.Je ulimpendea nini mpenzi wako wa zamani?
Kama jibu lako litakuwa, “sijui.” Mpenzi wako atakuwa hakuelewi, atadhani hata yeye hujui umempendea nini. Jaribu kumweleza yale ambayo yalikuvutia kwa mpenzi wako wa zamani lakini usitie chumvi, lakini ni nyema ukazungumzia zaidi sababu za kuachana kwenu, kwa mfano unaweza kumwambia kwamba, mpenzi wako alikuwa hapendi ujiendeleze kielimu au ulipopanda cheo hakufurahi akihisi utakuwa unatumia muda mwingi kazini wakati si kweli……… Jibu hilo litamfanya ajue msimamo wako linapokuja swala la kuendeleza kipaji chako….