|
Kamanda wa polisi akathibitisha tukio la ujambazi |
|
mambo ya kujiuzulu kwa viongozi |
|
loliondo ilikuwa ni stori kubwa sana nchin |
Nchini Tanzania suala la kukuta mtaa umefurika watu kwa ajili ya kushabikia au kuongelea kitu kimoja ni kawaida sana,yaani maofisini,mashuleni na hata safarini watu wanakuwa wakikijadili kitu hicho kimoja tu.Lakini kinachokuja kunishangaza mimi ni kuwa kitu hicho kinachojadiliwa kinadumu kwa muda mfupi sana midomoni mwa watu na baada ya hapo utadhani kwamba hakikuwahi kutukia.labda kama umesahau ngoja nikukumbushe enzi zile za ujambazi hapa nchini,kila siku vyombo vya habari vilikuwa vikiripoti matukio mbalmbali ya ujambazi hapa nchini kwetu na ikawa ndio wimbo wa taifa,baadae ikaja ufisadi!! ambao nao ukatawala sana midomoni mwa watu,haikukaa sana mara ikaja umeme,babu wa loliondo nae akavuma sana tena naweza sema yeye ndo kavunja rekodi ya stori zote kabla hajaanza kufifia kama si kupotea kabisa.Ndio leo hii ni wachache sana utawakuta wanaongelea habari za loliondo sasa sijui dawa imeisha au ndo ile kawaida yetu ya kushabikia kitu kwa muda tu na "kukipotezea"
|
ajali za barabarani |
|
migomo ya wanafunzi |
Hivi sasa karibu kila kona ya nchi utasikia habari za mgomo wa wauza mafuta.Hii ndo stori kubwa sana sasa ivi hapa nchini Tanzania.kwani wanafunzi,wafanyakazi na raia wengine wote wamesahau habari za dowans,loliondo.ufisadi.migomo ya wanafunzi udom na wanakumbuka tu habari za mafuta.....dah Sio mbaya na wala siwalaumu ila tu nimeipenda hii staili yetu hahahaha tunaishi,yaani tunaish i kwa setup,mpaka kitokee kitu ndio tupate mada
|
kupanda kwa bei ya mafuta,imekuwa ni stori kubwa mitaani |
Comments
Post a Comment
sema nasi hapa!!